Ndoto Ona pia Ufunuo Njia mojawapo ambayo Mungu hufunua mapenzi Yake kwa wanaume na wanawake duniani. Siyo ndoto zote ni mafunuo, hata hivyo. Ndoto za maongozi ya Mungu ni matunda ya imani. Akaota ndoto, na tazama ngazi imefika mbinguni, Mwa. 28:12. Yusufu akaota ndoto, Mwa. 37:5. Bwana atasema naye katika ndoto, Hes. 12:6. Nebukadneza aliota ndoto, Dan. 2:1–3. Wazee wataota ndoto, Yoe. 2:28 (Mdo. 2:17). Malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto, Mt. 1:20 (Mt. 2:19). Lehi aliandika mambo mengi aliyoyaona katika ndoto, 1 Ne. 1:16. Lehi aliota ndoto, 1 Ne. 8.