Katika Kitabu cha Mormoni, ni mwana wa Mfalme Mosia. Amoni aliyefanya kazi kama mmisionari ambaye bidii ya jitihada zake zilisaidia kuziongoa roho nyingi kwa Kristo.
Alikuwa mtu asiyeamini na aliyetafuta kuliangamiza Kanisa, Mos. 27:8–10, 34 .
Malaika alimtokea yeye na wenzi wake, Mos. 27:11 .
Akatubu na kuanza kulihubiri neno la Mungu, Mos. 27:32–28:8 .
Alikataa kuwa mfalme na badala yake alikwenda katika nchi ya Walamani kuhubiri neno la Mungu, Alma 17:6–9 .
Alifunga na kusali kwa ajili ya kupata mwongozo, Alma 17:8–11 .
Alichukuliwa akiwa amefungwa hadi kwa Mfalme Lamoni, Alma 17:20–21 .
Aliokoa kundi la mifugo ya Lamoni, Alma 17:26–39 .
Alimhubiria Lamoni, Alma 18:1–19:13 .
Alimshukuru Mungu na akazidiwa na shangwe, Alma 19:14 .
Aliowaongoa kamwe hawakuanguka, Alma 23:6 .
Alijawa shangwe kuwa chombo mikononi mwa Mungu cha kuwaleta maelfu kwenye ukweli, Alma 26:1–8 (Alma 26 ).
Aliwaongoza watu Anti-Nefi-Lehi kwenye usalama, Alma 27 .
Alijisikia shangwe kuu katika kukutana na Alma, Alma 27:16–18 .