Mafundisho na matendo ya Kanisa ambayo yanaonyesha kuwa limekubaliwa na Mungu na ni njia ambayo Bwana ameiweka kwa ajili ya watoto Wake kupata utimilifu wa baraka Zake. Baadhi ya ishara za Kanisa la kweli ni kama zifuatazo:
Kanuni na ibada za Kwanza
Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, Yn. 3:3–5 .
Tubuni na mkabatizwe, kila mmoja wenu, katika jina la Yesu Kristo, Mdo. 2:38 .
Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu, Mdo. 8:14–17 .
Mmekuwa watoto wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo, Gal. 3:26–27 .
Ukuhani sahihi unahitajika ili kubatiza na kutoa kipawa cha Roho Mtakatifu, JS—H 1:70–72 .
Kanuni na maagizo ya Kwanza ya injili yanaelezwa, M ya I 1:4 .
Mahali pasipo na maono, watu huangamia, Mit. 29:18 .
Bwana hufunua siri zake kwa manabii wake, Amo. 3:7 .
Nabii atapokea amri kwa ajili ya Kanisa, M&M 21:4–5 .
Hapana mtu atakaye hubiri injili au kujenga Kanisa isipokuwa yeye ametawazwa na mtu aliye na mamlaka, M&M 42:11 .
Wazee watahubiri injili, wakitenda hivyo kwa mamlaka, M&M 68:8 .
Maandiko nyongeza ya yatakuja
Kwa hiyo, enendeni, na mkawafundishe mataifa yote, Mt. 28:19–20 .
Sabini waliitwa ili kuhubiri injili, Lk. 10:1 .
Wazee watakwenda, wakiitangaza injili yangu, wawili wawili, M&M 42:6 .
Injili lazima ihubiriwe kwa kila kiumbe, M&M 58:64 .
Nitafanya agano nao na kuweka patakatifu pangu katikati yao milele daima, Eze. 37:26–27 .
Bwana atalijilia hekalu lake ghafla, Mal. 3:1 .
Watakatifu wanarudiwa kwa kushindwa kujenga nyumba ya Bwana, M&M 95 (M&M 88:119 ).
Watu wa Bwana daima walijenga mahekalu kwa ajili ya utendaji wa ibada takatifu, M&M 124:37–44 .
Kujenga mahekalu na kufanya ibada ni sehemu ya kazi kubwa ya siku za mwisho, M&M 138:53–54 .