Esta
Mwanamke wa imani kuu na mhusika mkuu katika kitabu cha Esta.
Kitabu cha Esta
Kitabu kilichoko katika Agano la Kale ambacho kina hadithi ya ujasiri mkuu wa Malkia Esta katika kuwaokoa watu wake kutokana na angamizo.
Mlango wa 1–2 hutuambia namna Esta, mwanamke wa Kiyahudi na binti wa kupanga wa mwanamume wa Kiyahudi aliyeitwa Mordekai, alichaguliwa kuwa Malkia wa Uajemi kwa sababu ya urembo wake. Mlango wa 3 unaelezea kwamba Hamani; kiongozi katika baraza la mfalme, alimchukia Mordekai na akafaulu kupata agizo kutoka kwa mfalme ya kuuawa kwa watu walio Wayahudi wote. Mlango wa 4–10 inaelezea namna Esta, kwa hatari kubwa ya maisha yake, aliifichua asili yake mwenyewe kwa mfalme na akafaulu kubadilisha agizo hilo.