Mtu mwenye kuokoa. Yesu Kristo, kwa njia ya upatanisho Wake, ametoa ukombozi na wokovu kwa wanadamu wote. Yesu Kristo ni Mwokozi wa wanadamu kwa sababu yeye aliwaokoa wote kutoka utumwa wa mauti na wenye kutubu kutokana na adhabu za dhambi. “Mwokozi” ni jina na cheo cha Yesu Kristo.
Utamwita jina lake Yesu: maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao, Mt. 1:21 .
Kwenu amezaliwa leo Mwokozi, ambaye ndiye Kristo Bwana, Lk. 2:11 .
Mungu aliupenda ulimwengu hata Mwanawe wa Pekee akaja kuwaokoa wanadamu, Yn. 3:16–17 .
Hapana jina jingine zaidi ya Kristo ambalo kwalo wanadamu wanaweza kuokolewa, Mdo. 4:10–12 (2 Ne. 25:20 ; Mos. 3:17 ; 5:8 ; M&M 18:23 ; Musa 6:52 ).
Mwokozi atakuja kutoka Sayuni, Rum. 11:26 .
Kutoka mbinguni tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo, Flp. 3:20 .
Baba amemtuma Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu, 1 Yoh. 4:14 .
Bwana amemwinua Masiya, Mwokozi wa ulimwengu, 1 Ne. 10:4 .
Mwanakondoo wa Mungu ndiye Mwokozi wa ulimwengu, 1 Ne. 13:40 .
Ufahamu juu ya Mwokozi utaenea kote katika kila taifa, koo, lugha na watu, Mos. 3:20 .
Kristo ilibidi afe ili wokovu uweze kuja, Hel. 14:15–16 .
Kuhesabiwa haki na utakaso kupitia Mwokozi ni haki na kweli, M&M 20:30–31 .
Mimi ndimi Yesu Kristo, Mwokozi wa ulimwengu, M&M 43:34 .
Watakatifu walimshukuru Mwana wa Mungu kama Mkombozi wao na Mwokozi wao, M&M 138:23 .
Mwanangu wa Pekee ndiye Mwokozi, Musa 1:6 .
Kadiri wengi watakavyoamini katika Mwana na kutubu dhambi zao wataokolewa, Musa 5:15 .