Yesu Kristo ndiye Mkombozi mkuu wa wanadamu kwa sababu Yeye, kupitia Upatanisho Wake, alilipia dhambi za wanadamu na akawezesha kupatikana kwa ufufuko wa watu wote.
Mtamwita jina lake Yesu: kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao, Mt. 1:21 .
Mwana wa Mtu amekuja kuutoa uhai wake kama fidia kwa ajili ya wengi, Mt. 20:28 (1 Tim. 2:5–6 ).
Bwana Mungu wa Israeli amewatembele na kuwakomboa watu wake, Lk. 1:68 .
Tulipatanishwa kwa Mungu kwa kifo cha Mwanawe, Rum. 5:10 .
Yesu Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu, ili apate kutukomboa na uovu wote, Tit. 2:13–14 .
Yesu Kristo alituosha dhambi zetu katika damu yake yeye mwenyewe, Ufu. 1:5 .
Ukombozi huja katika na kupitia Masiya Mtakatifu, 2 Ne. 2:6–7, 26 .
Mwana alijitwalia juu yake uovu na uvunjaji sheria wa wanadamu, akawakomboa, na akatosheleza madai ya haki, Mos. 15:6–9, 18–27 .
Kristo alikuja kuwakomboa wale wote ambao wangebatizwa ubatizo wa toba, Alma 9:26–27 .
Atakuja ulimwenguni kuwakomboa watu wake, Alma 11:40–41 .
Ukombozi huja kwa njia ya toba, Alma 42:13–26 .
Yesu alikuja kuukomboa ulimwengu, Hel. 5:9–12 .
Kristo amewakomboa wanadamu kutokana na kifo cha kimwili na kiroho, Hel. 14:12–17 .
Ukombozi huja kupitia kwa Kristo, 3Â Ne. 9:17 .
Mimi ndiye niliyetayarishwa tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu ili kuwakomboa watu wangu, Eth. 3:14 .
Bwana Mkombozi wenu aliteseka mauti katika mwili, M&M 18:11 .
Kristo aliteseka kwa ajili ya wote kama watatubu, M&M 19:1, 16–20 .
Watoto wadogo wamekombolewa kupitia Mwana wa Pekee, M&M 29:46 .
Nimempeleka Mwanangu wa Pekee katika ulimwengu kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu, M&M 49:5 .
Kristo ndiye nuru na Mkombozi wa ulimwengu, M&M 93:8–9 .
Joseph F. Smith alipokea ono juu ya wokovu wa wafu, M&M 138 .