Benjamini, Baba wa Mosia Ona pia Mosia, Mwana wa Benjamini Nabii katika Kitabu cha Mormoni na ni mfalme (Mos. 1–6). Alijishughulisha na matatizo makubwa katika kustawisha amani katika nchi, Omni 1:23–25 (M. ya Morm. 1:12–18). Aliwafundisha wanawe, Mos. 1:1–8. Aliuweka ufalme juu ya mwanawe Mosia, Mos. 1:9–18. Watu wake walikusanyika ili kusikiliza hotuba yake ya mwisho, Mos. 2:1–8. Aliwahutubia watu wake, Mos. 2:9–4:30. Watu wake walifanya agano na Bwana, Mos. 5–6.