Kusema uovu Ona pia Kusema uongo; Sengenya; Ushindani; Uvumi Kusema mambo ambayo siyo sahihi, yenye kuumiza, na yaliyo mabaya. Mara kwa mara katika maandiko misemo ya jinsi hii huelekezwa kwa mtu kwa dhamira maalumu ya kumsababishia maumivu. Uzuie ulimi wako na uovu, Zab. 34:13 (1 Pet. 3:10). Mtu asiye mchamungu huchimba uovu, Mit. 16:27. Heri ninyi watu watakapo wanenea kila neno ovu kwa uongo, Mt. 5:11 (3 Ne. 12:11). Moyoni hutoka mawazo maovu, Mt. 15:19 (Mk. 7:21). Usinene mabaya ya mtawala, Mdo. 23:5. Na maneno maovu yote yaondoke kwenu, Efe. 4:31. Msineneane uovu, Yak. (Bib.) 4:11. Angalieni kwamba hakuna masengenyo, wala kusema uovu, M&M 20:54.