Mtu kuwa mpole na mwenye kufundishika, au hali ya kuwa mpole na mwenye kufundishika. Unyenyekevu ni pamoja na kutambua utegemezi wetu kwa Mungu na kutamani kujiweka katika mapenzi Yake.
Mungu alikuongoza jangwani kwa miaka arobaini ili kukufanya uwe mnyenyekevu, Kum. 8:2 .
Niliinyenyekeza nafsi yangu kwa kufunga, Zab. 35:13 .
Heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu, Mh. 4:13 .
Bwana hukaa pamoja na yule aliye mnyenyekevu, Isa. 57:15 .
Unyenyekevu ni sifa kwa ajili ya ubatizo, M&M 20:37 .
Jinyenyekezeni mbele yangu na nanyi mtaniona na kujua ya kuwa Mimi ndimi, M&M 67:10 .
Uwe mnyenyekevu na Bwana atakupa jibu la sala zako, M&M 112:10 .
Mtu aliye mjinga na ajifunze hekima kwa kujinyenyekeza mwenyewe, M&M 136:32 .
Roho amepelekwa ili kuwaangaza walio wanyenyekevu, M&M 136:33 .