Madaraja ya Utukufu Ona pia Utukufu wa Selestia; Utukufu wa Telestia; Utukufu wa Terestria Tofauti za falme katika mbingu. Wakati wa Hukumu ya Mwisho, kila mtu atarithi mahali pake pa kuishi milele katika utukufu wa ufalme maalumu, isipokuwa wale walio wana wa Upotevu. Yesu alisema, Katika nyumba ya Baba yangu mna makao mengi, Yn. 14:2 (Eth. 12:32). Kuna utukufu mmoja wa jua, na mwingine wa mwezi, na mwingine wa nyota, 1 Kor. 15:40–41. Paulo alinyakuliwa juu katika mbingu ya tatu, 2 Kor. 12:2. Kuna mahali pasipokuwa na utukufu na penye adhabu isiyo na mwisho, M&M 76:30–38, 43–45. Kuna madaraja matatu ya utukufu, M&M 76:50–113; 88:20–32.