Misaada ya Kujifunza
Kipindi


Kipindi

Kipindi cha injili ni wakati ambamo ndani yake Bwana anakuwa na angalao mtumishi mmoja mwenye mamlaka hapa duniani mwenye kushikilia funguo za ukuhani mtakatifu.

Adamu, Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Musa, Yesu Kristo, Joseph Smith, na wengineo kila mmoja wao alianzisha kipindi kipya cha injili. Wakati Bwana aanzishapo kipindi, injili hufunuliwa upya ili watu wa kipindi hicho cha maongozi hawahitaji kutegemea vipindi vilivyopita kwa elimu ya mpango wa wokovu. Kipindi kilichoanzishwa na Joseph Smith kinajulikana kama “kipindi cha utimilifu wa nyakati.”