Subira Ona pia Pole, Upole; Stahimili Ustahimilivu wa utulivu; ni uwezo wa kustahimili mateso, matukano, au majeraha pasipo kulalamika au kulipiza. Tulia katika Bwana, na umngojee kwa subira, Zab. 37:7–8. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi, Mit. 14:29. Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu, Lk. 21:19. Tunalo tumaini kwa njia ya subira na faraja ya maandiko, Rum. 15:4. Mkawe wafuasi wa hao ambao kwa imani na subira huzirithi ahadi, Ebr. 6:12–15. Subira na iwe na kazi kamilifu, ili mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, Yak. (Bib.) 1:2–4. Mmesikia juu ya subira yake Ayubu, Yak. (Bib.) 5:11. Walitii kwa furaha na kwa subira mapenzi yote ya Bwana, Mos. 24:15. Nawe ulivumilia mambo haya yote kwa subira kwa sababu Bwana alikuwa pamoja nawe, Alma 38:4–5. Endeleeni katika subira hadi mtakapokuwa mmekamilika, M&M 67:13.