Njoo Ona pia Mtiifu, Tii, Utii; Mwanafunzi Katika maandiko, daima humaanisha kusogea karibu na mtu kwa kufuata au kutii, kama vile ilivyo katika usemi “njooni kwa Kristo, na mkakamilishwe ndani yake” (Moro. 10:32). Tegeni masikio yenu na kunijia, Isa. 55:3. Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao, Mt. 11:28. Waacheni watoto wadogo waje kwangu, Mt. 19:14. Kama mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, Lk. 9:23. Yeyote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, Yn. 6:35. Kristo anawaalika wote kuja kwake, 2 Ne. 26:33. Njooni kwangu na muokolewe, 3 Ne. 12:20. Njooni kwa Kristo, Moro. 10:32. Waalikeni wote waje kwa Kristo, M&M 20:59. Njooni kwangu, na nafsi zenu zitakuwa hai, M&M 45:46.