Kaini Ona pia Adamu; Habili; Makundi maovu ya siri; Mauaji Mwanawe Adamu na Hawa ambaye alimuua kaka yake mdogo Habili (Mwa. 4:1–16). Sadaka yake ilikataliwa na Bwana, Mwa. 4:3–7 (Musa 5:5–8, 18–26). Alimwua kaka yake Habili, Mwa. 4:8–14 (Musa 5:32–37). Bwana akaweka laana na alama juu yake, Mwa. 4:15 (Musa 5:37–41). Adamu na Hawa walikuwa na wana na mabinti wengi kabla ya kuzaliwa yeye, Musa 5:1–3, 16–17. Alimpenda Shetani zaidi kuliko Mungu, Musa 5:13, 18. Akaingia katika agano lisilo takatifu na Shetani, Musa 5:29–31.