Vita Ona pia Amani Pambano, au ugomvi wa silaha; kupigana kwa silaha. Bwana hukemea vita isipokuwa tu kama ndiyo njia ya mwisho kwa Watakatifu Wake ili kuzilinda familia zao, mali, haki, heshima na uhuru wao (Alma 43:9, 45–47). Moroni alitafuta kuwalinda watu wake, haki zake, nchi yake, na dini yake, Alma 48:10–17. Joseph Smith alipokea ufunuo na unabii juu ya vita, M&M 87. Kemeeni vita na tangazeni amani, M&M 98:16, 34–46. Tunaamini kwamba wanadamu huhesabiwa haki katika kujilinda wao wenyewe, marafiki zao, na mali, na serikali yao, M&M 134:11. Tunaamini katika kutii, kuheshimu, na kuunga mkono sheria, M ya I 1:12.