Bidii Msimamo thabiti, jitihada za ujasiri hasa katika kumtumikia Bwana na kutii neno Lake. Nisikilizeni kwa bidii, Isa. 55:2. Mungu ndiye mtoa thawabu kwao wale wamtafutao kwa bidii, Ebr. 11:6. Mkifanya bidii yote, katika imani yenu ongezeni na wema, 2 Pet. 1:5. Tulifundishe neno la Mungu kwa bidii yote, Yak. (KM) 1:19. Waliyapekua maandiko kwa bidii, Alma 17:2. Walitamani kwa bidii yote kushika amri, 3 Ne. 6:14. Tufanye kazi kwa bidii, Moro. 9:6. Jiingizeni kwa shauku katika kazi njema, M&M 58:27. Wala msikae bure pasipo kazi bali fanyeni kazi kwa nguvu zenu, M&M 75:3. Fanyeni bidii ya kuwa wasikivu kwa maneno ya uzima wa milele, M&M 84:43. Kila mtu na ajifunze wajibu wake, na kutenda kazi kwa bidii yote, M&M 107:99.