Kuabudu Ona pia Mungu, Uungu Kumpenda, kumnyenyekea, kumtumikia, na kujitoa kwa Mungu (M&M 20:19). Kuabudu kunajumuisha sala, kufunga, ibada ya kanisani, kushiriki katika ibada za injili, na matendo mengine yanayoonyesha kuabudu na upendo kwa Mungu. Usiwe na miungu wengine mbele yangu, Ku. 20:3 (Ku. 32:1–8, 19–35; Zab. 81:9). Watamwabudu Baba katika roho na katika kweli, Yn. 4:23. Mwabuduni yeye aliyezifanya mbingu na dunia, Ufu. 14:7 (M&M 133:38–39). Mwabuduni yeye kwa uwezo, akili, na nguvu zenu zote, 2 Ne. 25:29. Waliamini katika Kristo na walimwabudu Baba katika jina lake, Yak. (KM) 4:5. Zeno alifundisha kwamba watu wanapaswa kusali na kuabudu katika mahali pote, Alma 33:3–11. Mwabudu Bwana, katika mahali popote utakapokuwa, katika roho na katika kweli, Alma 34:38. Watu walianguka miguuni pa Yesu na wakamwabudu, 3 Ne. 11:17. Watu wote lazima watubu, wamwamini Yesu Kristo, na kumuabudu Baba katika jina lake, M&M 20:29. Ninawapa maneno haya ili mpate kufahamu na kujua namna ya kuabudu, na kujua nini mnachokiabudu, M&M 93:19. Ni Mungu huyu mmoja tu ndiye nitakayemwabudu, Musa 1:12–20. Tunadai haki ya kumwabudu Mwenyezi Mungu, M ya I 1:11.