Utambuzi, Kipawa cha Ona pia Vipawa vya Roho Kufahamu au kujua kitu fulani kwa njia ya uwezo wa Roho. Kipawa cha utambuzi ni moja ya vipawa vya Roho. Inajumuisha kutambulika kwa tabia za kweli za watu na chanzo na maana ya maonyesho ya kiroho. Mwanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo, 1Â Sam. 16:7. Ole wao waitao uovu kuwa ni wema, Isa. 5:20 (2Â Ne. 15:20). Mambo ya Mungu yatambulika kwa jinsi ya rohoni, 1Â Kor. 2:14. Kwa watu wengine kimetolewa kipawa cha utambizi wa roho, 1Â Kor. 12:10. Amoni angeweza kutambua mawazo yake, Alma 18:18. Ile sauti ndogo tulivu iliwapenya wale walioisikia, 3Â Ne. 11:3. Ili msipate kudanganyika, zitakeni karama zilizo bora, M&M 46:8, 23. Viongozi wa Kanisa hupewa uwezo wa kutambua vipawa vya Roho, M&M 46:27. Ule mwili uliojazwa na nuru hufahamu mambo yote, M&M 88:67. Musa aliitazama dunia, na akaitambua kwa uwezo wa Roho wa Mungu, Musa 1:27.