Nikodemo Ona pia Mafarisayo Katika Agano Jipya, ni mtawala mwadilifu wa Wayahudi (labda wa Sanhedrini) na Mfarisayo (Yn. 3:1). Aliongea na Yesu usiku, Yn. 3:1–21. Alimtetea Yesu kwa Mafarisayo, Yn. 7:50–53. Alileta manukato katika mazishi ya Yesu, Yn. 19:39–40.