Misaada ya Kujifunza
Roho Mtakatifu


Roho Mtakatifu

Mshirika wa tatu wa Uungu (1 Yoh. 5:7; M&M 20:28). Yeye ni mtu wa Roho, hana mwili wa nyama na mifupa (M&M 130:22). Roho Mtakatifu mara nyingi hutajwa kama Roho, au Roho wa Mungu.

Roho Mtakatifu hufanya kazi kadhaa zilizo muhimu katika mpango wa wokovu. (1) Hutoa ushuhuda juu ya Baba na Mwana (1 Kor. 12:3; 3 Ne. 28:11; Eth. 12:41). (2) Hutufunulia ukweli wa mambo yote (Yn. 14:26; 16:13; Moro. 10:5; M&M 39:6). (3) Huwatakasa wale waliotubu na kubatizwa (Yn. 3:5; 3 Ne. 27:20; Musa 6:64–68). (4) Yeye ndiye Roho Mtakatifu wa Ahadi (M&M 76:50–53; 132:7, 18–19, 26).

Uwezo wa Roho Mtakatifu waweza kuja juu ya mtu kabla ya ubatizo na kumshuhudia kwamba injili ni ya kweli. Lakini haki ya kuwa na Roho Mtakatifu wakati wote, mtu anapokuwa mwenye kustahili, ni karama ambayo inaweza kupokelewa tu kwa kuwekewa mikono na mtu mwenye Ukuhani wa Melkizedeki baada ya kubatizwa na mtu aliye na mamlaka katika Kanisa la kweli la Yesu Kristo.

Yesu alifundisha kwamba dhambi zote zaweza kusamehewa isipokuwa kumkufuru Roho Mtakatifu (Mt. 12:31–32; Mk. 3:28–29; Lk. 12:10; Ebr. 6:4–8; M&M 76:34–35).