Kukufuru, Kufuru
Kuongea bila heshima au staha juu ya Mungu au vitu vitakatifu.
Yesu alituhumiwa mara kadhaa na Wayahudi kwa madai ya kukufuru kwa sababu Yeye alidai haki ya kusamehe dhambi (Mt. 9:2–3; Lk. 5:20–21), kwa sababu Yeye alijiita Mwenyewe kuwa ni Mwana wa Mungu (Yn. 10:22–36; 19:7), na kwa sababu Yeye alisema wao watamwona Yeye ameketi mkono wa kuume wa nguvu na kuja juu ya mawingu ya mbinguni (Mt. 26:64–65). Tuhuma hizi zingekuwa kweli kama Yeye hakika Hakuwa kile Alichosema Alikuwa. Tuhuma ililetwa dhidi Yake na mashahidi waongo katika kesi mbele ya Sanhedrini (Mt. 26:59–61) ilikuwa kukufuru dhidi ya hekalu la Mungu. Kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu, ambavyo ni kumkana Kristo makusudi baada ya kupokea elimu kamili juu Yake ni dhambi isiyosameheka (Mt. 12:31–32; Mk. 3:28–29; M&M 132:27).