Kutoa maarifa kwa wengine, hususani juu ya kweli za injili, na kuwaongoza katika uadilifu. Watu wanaofundisha injili yawapasa kuongozwa na Roho. Wazazi wote ni walimu ndani ya familia zao wenyewe. Watakatifu wanapaswa kuomba na kuwa radhi kukubali mafundisho kutoka kwa Bwana na viongozi Wake.
Twajua ya kuwa yu mwalimu kutoka kwa Mungu, Yn. 3:2 .
Basi wewe umfundishaye mwingine, je, hujifundishi mwenyewe, Rum. 2:21 .
Nilikuwa nimefundishwa kiasi fulani katika mafundisho yote ya baba yangu, 1Â Ne. 1:1 (Eno. 1:1 ).
Makuhani na walimu lazima wafundishe kwa bidii au wajibu dhambi za watu juu ya vichwa vyao, Yak. (KM) 1:18–19 .
Nisikilizeni, na mfungue masikio yenu, Mos. 2:9 .
Mtawafundisha watoto wenu kupendana na kutumikiana, Mos. 4:15 .
Msimwamini yeyote kuwa mwalimu wenu isipokuwa amekuwa mtu wa Mungu, Mos. 23:14 .
Bwana aliimwaga roho yake juu ya nchi yote ili kuitayarisha mioyo yao kulipokea neno, Alma 16:16 .
Walifundisha kwa nguvu na mamlaka ya Mungu, Alma 17:2–3 .
Walikuwa wamefundishwa na mama zao, Alma 56:47 (Alma 57:21 ).
Kadiri watakavyoitafuta hekima waweze kuelekezwa, M&M 1:26 .
Fundishaneni kulingana na ofisi ambayo ninawateua, M&M 38:23 .
Fundisha kanuni za injili yangu, ambazo zimo katika Biblia na Kitabu cha Mormoni, M&M 42:12 .
Mtafundishwa kutoka juu, M&M 43:15–16 .
Wazazi watawafundisha watoto wao, M&M 68:25–28 .
Fundishaneni mafundisho ya ufalme, M&M 88:77–78, 118 .
Chagueni miongoni mwenu mwalimu, M&M 88:122 .
Hujawafundisha watoto wako nuru na kweli, na hii ndiyo chanzo cha mateso yako, M&M 93:39–42 .
Si ninyi msemao, bali ni Roho asemaye ndani yenu, Mt. 10:19–20 .
Je, mioyo yetu haikuwaka ndani yetu wakati alipotufungulia maandiko, Lk. 24:32 .
Injili inahubiriwa kwa uwezo wa Roho, 1 Kor. 2:1–14 .