Kazi ya kimisionari Ona pia Hubiri; Injili Kuhubiri injili ya Yesu Kristo kwa neno na kwa mfano. Jinsi gani ilivyo mizuri juu ya milima miguu yake yeye autangazaye, wokovu, Isa. 52:7. Nitawatafuta kondoo wangu na kuwaulizia, Eze. 34:11. Mkaihubiri injili kwa kila kiumbe, Mk. 16:15 (Morm. 9:22). Mashamba ni meupe tayari kwa mavuno, Yn. 4:35. Na watahubirije pasipo kupelekwa, Rum. 10:15. Wafundisheni neno la Mungu kwa bidii yote, Yak. (KM) 1:19. Bwana huwakubalia mataifa yote kufundisha neno lake, Alma 29:8. Injili ipate kutangazwa na watu walio dhaifu na wa kawaida, M&M 1:23. Kazi ya ajabu i karibu kuanza, M&M 4:1. Kama utafanya kazi katika siku zako zote na kuileta, japo iwe nafsi moja kwangu, shangwe yako ni kuu namna gani! M&M 18:15. Wateule wangu huisikia sauti yangu na hawaishupazi mioyo yao, M&M 29:7. Enendeni mkiihubiri injili yangu, wawili wawili, M&M 42:6. Sauti lazima iende kutoka mahali hapa, M&M 58:64. Mfungue vinywa vyenu katika kuitangaza injili yangu, M&M 71:1. Tangazeni ukweli kulingana na mafunuo na amri, M&M 75:4. Kila mtu aliyeonywa anapaswa amwonye jirani yake, M&M 88:81 (M&M 38:40–41). Bwana atazitunza familia za wale wanaohubiri injili, M&M 118:3. Watumishi wa Bwana watakwenda mbele, M&M 133:38. Wazee walio waaminifu, wanapoondoka kutoka maisha haya ya kufa, huendelea kufanya kazi zao, M&M 138:57.