Amri Kumi
Sheria kumi zilizotolewa na Mungu kupitia nabii Musa ili kudhibiti tabia za kimwili.
Jina la Kiebrania kwa amri hizi ni “Maneno Kumi.” Pia zinaitwa Agano (Kum. 9:9) au ushuhuda (Ku. 25:21; 32:15). Namna Mungu alivyotoa Amri Kumi kwa Musa, na kupitia yeye kwenda kwao Waisraeli, inaelezwa katika Ku. 19:9–20:23; 32:15–19; 34:1. Amri hizi zilikuwa zimechongwa juu ya mabamba mbili ya mawe, ambazo ziliwekwa katika Sanduku; kwa sababu hiyo Sanduku hilo liliitwa Sanduku la Agano (Hes. 10:33). Bwana, akinukuu kutoka Kum. 6:4–5 na Law. 19:18 amezifupisha Amri Kumi hizi katika “amri kuu mbili” (Mt. 22:37–39).
Amri kumi hizi zimerudiwa tena katika ufunuo wa siku za mwisho (TJS, Ku. 34:1–2, 14 [Kiambatisho]; Mos. 12:32–37; 13:12–24; M&M 42:18–28; 59:5–13).