Huruma Ona pia Hisani; Rehema, enye Rehema; Upendo Katika maandiko, huruma kwa maana halisi humaanisha “kuteseka pamoja na.” Pia inamaanisha ni kuonyesha utu wema, kusikitika, na rehema kwa mtu mwingine. Bwana aliwaagiza watu wake kuonyesha huruma, Zek. 7:8–10. Yesu aliwahurumia, Mt. 9:36 (Mt. 20:34; Mk. 1:41; Lk. 7:13). Msamaria mmoja alimhurumia, Lk. 10:33. Mhurumiane, 1 Pet. 3:8. Kristo amejawa na huruma kwa watoto wa watu, Mos. 15:9. Matumbo yangu yamejawa na huruma juu yenu, 3 Ne. 17:6. Joseph Smith alisali kwa ajili ya huruma ya Bwana, M&M 121:3–5.