Chuki, Chukia Ona pia Kisasi; Uadui; Upendo Chukia ni hali yenye nguvu ya kutompenda mtu fulani au kitu fulani. Mimi, Mungu huupatiliza uovu wa baba juu ya watoto wao wale wanichukiao, Ku. 20:5. Mambo haya sita Bwana huyachukia, Mit. 6:16. Mtu mjinga humdharau mama yake, Mit. 15:20. Amedharauliwa na kukataliwa na wanadamu, Isa. 53:3. Watendeeni mema wale wanao wachukia, Mt. 5:44. Ama atamchukia mmoja na kupenda mwingine, au atashikamana na mmoja, na kumdharau mwingine, Mt. 6:24. Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, Mt. 10:22. Kila mtu atendaye uovu huichukia nuru, Yn. 3:20. Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, 1 Tim. 4:12. Kwa sababu wao ni matajiri, wanawadharau maskini, 2 Ne. 9:30. Usidharau mafunuo ya Mungu, Yak. (KM) 4:8. Walikuwa na chuki ya milele dhidi yetu, Yak. (KM) 7:24. Wanadamu waliyapuuza mashauri ya Mungu, na kudharau maneno yake, M&M 3:7. Nilichukiwa na kuteswa kwa kusema kwamba niliona ono, JS—H 1:25.