Dhambi isiyo sameheka Ona pia Kukufuru, Kufuru; Mauaji; Roho Mtakatifu; Wana wa Upotevu Dhambi ya kumkana Roho Mtakatifu, ni dhambi ambayo haiwezi kusamehewa. Kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu haitasamehewa kwa wanadamu, Mt. 12:31–32 (Mk. 3:29; Lk. 12:10). Haiwezekani kwa wale waliofanywa washiriki wa Roho Mtakatifu kuwafanya upya tena hata katika toba, Ebr. 6:4–6. Kama tutafanya dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ukweli haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi, Ebr. 10:26. Kama mtamkana Roho Mtakatifu na ukajua kwamba unamkana, hii ni dhambi ambayo isiyosameheka, Alma 39:5–6 (Yak. [KM] 7:19). Hawana msamaha, wakiwa wamemkana Mwana wa Pekee, wakiwa wanamsulubisha kwa nafsi zao, M&M 76:30–35. Kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu haitasamehewa, ambayo ni kumwaga damu isiyo na hatia baada ya kupokea agano langu jipya na lisilo na mwisho, M&M 132:26–27.