Heshima Ona pia Tukuza; Uchaji Kama kawaida litumikavyo katika maandiko, kuonyesha staha na uchaji kwa mtu fulani au kitu fulani. Waheshimu baba yako na mama yako, Ku. 20:12 (1 Ne. 17:55; Mos. 13:20). Mheshimu Bwana kwa mali zako, Mit. 3:9. Kama mtu yeyote atanitumikia mimi, Baba yangu atamheshimu mtu huyo, Yn. 12:26. Waume yawapasa kuwaheshimu wake zao, 1 Pet. 3:7. Humheshimu Bwana kwa midomo yao tu, 2 Ne. 27:25 (Isa. 29:13). Sitafuti heshima ya ulimwengu, Alma 60:36. Ibilisi aliniasi, akisema, Nipe mimi heshima yako, ambayo ndiyo uwezo wangu, M&M 29:36. Walio waaminifu watavikwa taji la heshima, M&M 75:5 (M&M 124:55). Bwana hufurahi kuwapa heshima wale wamtumikiaye, M&M 76:5. Hawakuchaguliwa kwa sababu wao wanatafuta heshima ya wanadamu, M&M 121:34–35. Tunaamini katika kuheshimu na kuziunga mkono sheria, M ya I 1:12 (M&M 134:6).