Rehema, enye Rehema Ona pia Haki, Uadilifu, enye Uadilifu; Lipia dhambi, Upatanisho; Neema; Samehe; Yesu Kristo Roho ya huruma, upole, na msamaha. Rehema ni moja ya sifa za Mungu. Yesu Kristo hutoa rehema kwetu kupitia dhabihu Yake ya kutulipia dhambi. Bwana ni mwingi wa rehema na mwenye fadhili, Ku. 34:6 (Kum. 4:31). Rehema yake hudumu milele, 1 Nya. 16:34. Wema na fadhili zitanifuata, Zab. 23:6. Mtu mwenye huruma juu ya maskini ana heri, Mit. 14:21. Nataka fadhili wala si dhabihu, Hos. 6:6. Heri wenye rehema: maana hao watapata rehema, Mt. 5:7 (3 Ne. 12:7). Ole wenu wanafiki mlipao zaka na kuacha mambo makuu ya sheria, hukumu, rehema, na imani, Mt. 23:23. Basi muweni na rehema, kama Baba yenu pia alivyo na rehema, Lk. 6:36. Siyo kwa matendo yetu yaliyo ya haki, bali kulingana na rehema zake ametukomboa sisi, Tit. 3:5. Rehema za upendo wa Bwana zi juu ya wote, 1 Ne. 1:20. Rehema haina madai juu ya asiyetubu, Mos. 2:38–39. Mungu ni mwenye huruma kwa wote wenye kuamini katika jina lake, Alma 32:22. Rehema yaweza kuridhisha mahitaji ya haki, Alma 34:16. Je, wadhani rehema yaweza kumwibia haki, Alma 42:25 (Alma 42:13–25). Watoto wadogo wako hai katika Kristo kwa sababu ya rehema zake, Moro. 8:19–20 (M&M 29:46). Mkono wa rehema wa Yesu Kristo umelipia dhambi zenu, M&M 29:1. Kwa wema wa damu niliyoitoa, nimeomba mbele za Baba kwa ajili yao wanao liamini jina langu, M&M 38:4. Wale waliolishika agano langu watapata rehema, M&M 54:6. Mimi, Bwana, husamehe dhambi, na ni mwingi wa rehema kwa wale wenye kukiri dhambi zao kwa moyo mnyenyekevu, M&M 61:2. Mimi, Bwana, huonyesha huruma kwa wote walio wapole, M&M 97:2. Na mtu akupokeaye wewe kama mtoto mdogo, huupokea ufalme wangu, kwa maana watapata rehema, M&M 99:3. Neema itakwenda mbele ya uso wako, Musa 7:31.