Waanti-Nefi-Lehi Ona pia Amoni, Mwana wa Mosia; Helamani, Wana wa; Mosia, Wana wa Katika Kitabu cha Mormoni, ni jina lililotolewa kwa Walamani walioongolewa na wana wa Mosia. Baada ya wongofu wao, watu hawa, ambao pia waliitwa watu wa Amoni, waliendelea kuwa waaminifu katika maisha yao yote (Alma 23:4–7, 16–17; 27:20–27). Walichukua jina la Waanti-Nefi-Lehi, Alma 23:16–17; 24:1. Walikataa kumwaga damu na wakazika silaha zao, Alma 24:6–19. Watoto wao wa kiume walijiandaa kwa vita nao wakamchagua Helamani kama kiongozi wao, Alma 53:16–19; 56–58 (wana hawa pia walijulikana kama askari wa vita vijana 2,000).