Kuabudu sanamu Ibada ya masanamu au upenzi uliopita kiasi au upendo kwa kitu chochote. Usiwe na miungu mingine ila mimi, Ku. 20:3 (Mos. 12:35; 13:12–13). Ikiwa mtaandama na miungu mingine, hakika mtaangamia, Kum. 8:19. Ukaidi ni kama dhambi na kuabudu masanamu, 1 Sam. 15:23. Umejifunua nafsi yako kwa mwingine kuliko Mimi, Isa. 57:8. Umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu, Dan. 5:23. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali, Mt. 6:24. Tamaa mbaya ndiyo ibada ya sanamu, Kol. 3:5. Watoto, jilindeni nafsi zenu na sanamu, 1 Yoh. 5:21. Ole wao wale waabuduo masanamu, 2 Ne. 9:37. Kuabudu sanamu kwa watu wa Nefi kuliwaletea juu yao vita na maangamizo yao, Alma 50:21. Kila mtu anaenenda akifuata sura ya Mungu wake mwenyewe, M&M 1:16. Acha wafanye kazi kwa mikono yao wenyewe ili pasiwepo na kuabudu sanamu, M&M 52:39. Baba yake Ibrahimu alitekwa na ibada ya sanamu, Ibr. 1:27.