Ulimwengu Ona pia Babeli, Babilonia; Dunia; Hali ya Kufa, enye Kufa Dunia; mahali pa majaribu kwa wanadamu wenye miili ya kufa. Kama ishara, hutumika kwa wale watu ambao hawatii amri za Mungu. Maisha ya kuishi duniani Katika ulimwengu mtapata dhiki, Yn. 16:33. Msiogope hata kama itabidi kufa; kwani katika ulimwengu huu shangwe yenu siyo kamilifu, M&M 101:36. Watu wasiotii amri Nitauadhibu ulimwengu kwa sababu ya uovu wake, Isa. 13:11 (2 Ne. 23:11). Kama ulimwengu utawachukia, ninajua ya kuwa ulinichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi, Yn. 15:18–19. Jumba kubwa na pana lilikuwa ni kiburi cha ulimwengu, 1 Ne. 11:36. Ulimwengu unaiva katika uovu, M&M 18:6. Ujilinde na mawaa kutoka ulimwenguni, M&M 59:9. Yule aliye mwaminifu na mwenye kustahmili ataushinda ulimwengu, M&M 63:47. Hamtaishi kwa jinsi ya ulimwengu, M&M 95:13. Mwisho wa ulimwengu Ninaumba dunia mpya: na ya kwanza haitakumbukwa, Isa. 65:17 (Ufu. 21:1; M ya I 1:10). Katika mwisho wa ulimwengu huu, magugu yatakusanywa na kuchomwa katika moto, Mt. 13:40, 49 (Mal. 4:1; Yak. [KM] 6:3). Nitafanya shamba langu la mizabibu lichomwe kwa moto, Yak. (KM) 5:77 (M&M 64:23–24). Bwana atamwangamiza Shetani na kazi zake mwisho wa ulimwengu, M&M 19:3. Dunia itakufa, lakini itahuishwa tena, M&M 88:25–26. Bwana alimwonyesha Henoko mwisho wa ulimwengu, Musa 7:67.