Katika maandiko, amani yaweza kumaanisha uhuru kutokana na kutokuwepo ugomvi na misukosuko au utulivu na faraja ya ndani inayoletwa na Roho Mtakatifu ambayo Mungu huwapa Watakatifu Wake walio waaminifu.
Uhuru kutokana na ugomvi na misukosuko
Amani kutoka kwa Mungu kwa watiifu
Kulikuwa na jeshi la mbinguni, likimsifu Mungu na kusema, Utukufu kwa Mungu juu, na amani duniani, Lk. 2:13–14 .
Amani nawaachieni, Yn. 14:27 .
Amani ya Mungu ipitayo akili zote, Flp. 4:7 .
Watu wa Mfalme Benjamini walipata amani katika dhamira zao, Mos. 4:3 .
Jinsi gani ilivyo mizuri juu ya milima miguu yao watangazao amani, Mos. 15:14–18 (Isa. 52:7 ).
Alma alilia kwa Bwana na akapata amani, Alma 38:8 .
Roho za walio waadilifu hupokelewa katika hali ya amani, Alma 40:12 .
Sikusema amani akilini mwako kuhusiana na jambo hili, M&M 6:23 .
Enenda katika unyenyekevu wa Roho wangu, nawe utapata amani, M&M 19:23 .
Yule afanyaye kazi za haki atapokea amani, M&M 59:23 .
Jivikeni wenyewe kwa kifungo cha hisani, ambacho ni kifungo cha ukamilifu na amani, M&M 88:125 .
Mwanangu, amani iwe moyoni mwako, M&M 121:7 .