Ita, Itwa na Mungu, Wito Ona pia Alichagua, Chagua, Chaguliwa (kitenzi); Kutawaza, Kutawazwa; Mamlaka; Msimamizi, Usimamizi; Teule, Wateule Kuitwa na Mungu ni kupokea uteuzi au mwaliko kutoka Kwake au kiongozi Wake wa Kanisa aliye na mamlaka kisheria ya kumtumikia Yeye katika njia husika. Akaweka mikono yake na akampa mausia, Hes. 27:23. Nimekutawaza kuwa nabii, Yer. 1:5. Nimewachagua ninyi na kuwatawaza, Yn. 15:16. Paulo aliitwa kuwa Mtume, Rum. 1:1. Hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yule aliyeitwa na Mungu, Ebr. 5:4. Yesu aliitwa na Mungu kwa mfano wa Melkizedeki, Ebr. 5:10. Nimeitwa kulihubiri neno la Mungu kulingana na roho wa ufunuo na unabii, Alma 8:24. Makuhani waliitwa na kutayarishwa tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu, Alma 13:3. Kama unayo hamu ya kumtumikia Mungu, umeitwa, M&M 4:3. Simama imara katika kazi niliyokuitia, M&M 9:14. Usidhani kwamba umeitwa kuhubiri, hadi pale utakapoitwa, M&M 11:15. Wazee wameitwa kutimiza kusanyiko la wateule, M&M 29:7. Hakuna atakaye hubiri injili yangu au kulijenga Kanisa langu isipokuwa ametawazwa, M&M 42:11. Walioitwa ni wengi, lakini wateule ni wachache, M&M 121:34. Mtu lazima aitwe na Mungu, M ya I 1:5.