Takatifu Ona pia Safi na Isiyo safi; Utakaso; Utakatifu Kuwa na tabia ya kumchamungu, au kuwa safi kiroho na kimwili. Kinyume cha mtakatifu ni kuwa wa ulimwengu au kuwa mchafu. Mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu, Ku. 19:5–6 (1 Pet. 2:9). Bwana akamwamuru Israeli: Kuweni watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu, Law. 11:44–45. Wale walio na mikono safi na moyo safi watasimama katika mahali pake patakatifu, Zab. 24:3–4. Watawafundisha watu wangu tofauti kati ya vitu vitakatifu na vitu vichafu, Eze. 44:23. Mungu ametuita kwa wito mtakatifu, 2 Tim. 1:8–9. Tangu utoto umeyajua maandiko, 2 Tim. 3:15. Wanadamu watakatifu wa Mungu walinena kama walivyoongozwa na Roho Mtakatifu, 2 Pet. 1:21. Wanadamu wote watahukumiwa kulingana na ukweli na utakatifu ulioko katika Mungu, 2 Ne. 2:10. Mwanadamu wa asili huwa mtakatifu kupitia upatanisho wa Kristo, Mos. 3:19. Tembea kwa mfano mtakatifu wa Mungu, Alma 7:22 (Alma 13:11–12). Wanafunzi watatu walitakaswa katika mwili na wakafanywa kuwa watakatifu, 3 Ne. 28:1–9, 36–39. Usicheze na mambo matakatifu, M&M 6:12. Huwezi kuandika lililo takatifu isipokuwa limetolewa kwako kutoka kwangu, M&M 9:9. Mtajifunga ninyi wenyewe ili kutenda katika utakatifu wote, M&M 43:9. Wanafunzi wangu watasimama katika mahali patakatifu, M&M 45:32. Kile kijacho kutoka juu ni kitakatifu, M&M 63:64. Watoto wadogo ni watakatifu, M&M 74:7. Wekeni wakfu mahali pale napo patafanywa kuwa patakatifu, M&M 124:44. Bwana atawakusanya wateule wake katika mji mtakatifu, Musa 7:62.