Ona pia Alfa na Omega ; Amini, Imani ; Anguko la Adamu na Hawa ; Bwana ; Bwana Harusi ; Damu ; Dhabihu ; Dhamiri ; Golgotha ; Imanueli ; Injili, Vitabu vya Biblia ; Jiwe la pembeni ; Komboa, Kombolewa, Ukombozi ; Kugeuka sura—Kugeuka sura kwa Kristo ; Kupaa ; Kusulubiwa ; Lipia dhambi, Upatanisho ; Mahubiri ya Mlimani ; Maji ya Uzima ; Maria, Mama wa Yesu ; Masiya ; Mchungaji Mwema ; Mfariji ; Mimi Niko ; Mkate wa Uzima ; Mkombozi ; Mpakwa mafuta ; Mpango wa Ukombozi ; Mpatanishi ; Msalaba ; Mtetezi ; Mungu, Uungu ; Mwamba ; Mwana wa Mtu ; Mwanakondoo wa Mungu ; Mwanzo ; Mwokozi ; Mzaliwa wa Kwanza ; Neema ; Njia ; Nuru, Nuru ya Kristo ; Nyoka wa shaba nyeupe ; Ondoleo la Dhambi ; Sakramenti ; Siyo na mwisho ; Toba, Tubu ; Ufufuko ; Ujio wa Pili wa Yesu Kristo ; Umba, Uumbaji ; Yehova ; Zaliwa
Kristo (neno la Kiyunani) na Masiya (neno la Kiebrania) maana yake ni “mpakwa mafuta.” Yesu Kristo ndiye Mzaliwa wa kwanza wa Baba katika roho (Ebr. 1:6 ; M&M 93:21 ). Yeye ndiye Mzaliwa Pekee wa Baba katika mwili (Yn. 1:14 ; 3:16 ). Yeye ndiye Yehova (M&M 110:3–4 ) na aliteuliwa katika wito wake mkuu kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Chini ya maelekezo ya Baba, Yesu aliumba dunia na kila kitu kilichopo juu yake (Yn. 1:3, 14 ; Musa 1:31–33 ). Alizaliwa na Maria huko Bethlehemu, aliishi maisha yasiyo na dhambi, na akafanya upatanisho kamili kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote kwa kumwaga damu Yake na kwa kutoa uhai Wake juu ya msalaba (Mt. 2:1 ; 1 Ne. 11:13–33 ; 3 Ne. 27:13–16 ; M&M 76:40–42 ). Akafufuka kutoka kwa wafu, hivyo akathibitisha hatima ya kufufuka kwa wanadamu wote. Kupitia Upatanisho na Ufufuko wa Yesu, wale wanaotubu dhambi zao na kutii amri za Mungu wanaweza kuishi milele pamoja na Yesu na Baba (2 Ne. 9:10–12 ; 21–22 ; M&M 76:50–53, 62 ).
Yesu Kristo ndiye mtu mkuu kuliko wote waliozaliwa juu ya dunia. Maisha Yake ni mfano kamili wa jinsi wanadamu wote itupasavyo kuishi. Sala, baraka, na ibada zote za ukuhani zinapaswa kufanyika katika jina Lake. Yeye ni Bwana wa mabwana, Mfalme wa wafalme, Muumba, Mwokozi, na Mungu wa dunia nzima.
Yesu Kristo atakuja tena katika uwezo na utukufu ili kutawala juu ya dunia wakati wa Milenia. Katika siku ya mwisho, yeye atawahukumu wanadamu wote (Alma 11:40–41 ; JS—M 1 ).
Muhtasari wa maisha Yake (katika mfuatano wa matukio)
Kuzaliwa na huduma ya Yesu vilitabiriwa, Lk. 1:26–38 (Isa. 7:14 ; 9:6–7 ; 1 Ne. 11 ).
Alizaliwa, Lk. 2:1–7 (Mt. 1:18–25 ).
Alitahiriwa, Lk. 2:21 .
Aliletwa hekaluni, Lk. 2:22–38 .
Alitembelewa na mamajusi, Mt. 2:1–12 .
Yusufu na Maria walikimbia pamoja naye hadi Misri, Mt. 2:13–18 .
Aliletwa Nazarathi, Mt. 2:19–23 .
Alitembelea hekaluni katika umri wa miaka kumi na miwili, Lk. 2:41–50 .
Alikuwa na kaka na dada zake, Mt. 13:55–56 (Mk. 6:3 ).
Alibatizwa, Mt. 3:13–17 (Mk. 1:9–11 ; Lk. 3:21–22 ).
Alijaribiwa na ibilisi, Mt. 4:1–11 (Mk. 1:12–13 ; Lk. 4:1–13 ).
Aliwaita wanafunzi wake, Mt. 4:18–22 (Mt. 9:9 ; Mk. 1:16–20 ; 2:13–14 ; Lk. 5:1–11, 27–28 ; 6:12–16 ; Yn. 1:35–51 ).
Aliwapa mamlaka wale Kumi na Wawili, Mt. 10:1–4 (Mk. 3:13–19 ; Lk. 6:12–16 ).
Alitoa Mahubiri ya Mlimani, Mt. 5–7 .
Alitabiri mauti yake na ufufuko, Mt. 16:21 (Mt. 17:22–23 ; 20:17–19 ; Mk. 8:31 ; 9:30–32 ; 10:32–34 ; Lk. 9:22 ; 18:31–34 ).
Aligeuka sura, Mt. 17:1–9 (Mk. 9:2–8 ; Lk. 9:28–36 ).
Aliwatuma wale sabini, Lk. 10:1–20 .
Aliingia Yerusalemu kwa shangwe, Mt. 21:1–11 (Mk. 11:1–11 ; Lk. 19:29–40 ; Yn. 12:12–15 ).
Alianzisha sakramenti, Mt. 26:26–29 (Mk. 14:22–25 ; Lk. 22:19–20 ).
Aliteseka na kusali katika Gethsemani, Mt. 26:36–46 (Mk. 14:32–42 ; Lk. 22:39–46 ).
Alisalitiwa, kukamatwa, na kukimbiwa, Mt. 26:47–56 (Mk. 14:43–53 ; Lk. 22:47–54 ; Yn. 18:2–13 ).
Alisulubiwa, Mt. 27:31–54 (Mk. 15:20–41 ; Lk. 23:26–28, 32–49 ; Yn. 19:16–30 ).
Alifufuka, Mt. 28:1–8 (Mk. 16:1–8 ; Lk. 24:1–12 ; Yn. 20:1–10 ).
Alionekana baada ya ufufuko wake, Mt. 28:9–20 (Mk. 16:9–18 ; Lk. 24:13–48 ; Yn. 20:11–31 ; Mdo. 1:3–8 ; 1 Kor. 15:5–8 ).
Alipaa mbinguni, Mk. 16:19–20 (Lk. 24:51–53 ; Mdo. 1:9–12 ).
Kujichukulia jina la Yesu Kristo juu yetu
Hakuna jina jingine litupasalo sisi kuokolewa kwalo, Mdo. 4:12 (2 Ne. 31:21 ).
Mitume walifurahi kwa sababu walihesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake, Mdo. 5:38–42 .
Hii ndiyo amri yake, Kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, 1 Yoh. 3:23 .
Mtashuhudia ya kwamba mko radhi kujichukulia juu yenu jina la Kristo kwa ubatizo, 2 Ne. 31:13 .
Ningeliwataka ninyi mjichukulie juu yenu jina la Kristo, Mos. 5:6–12 (Mos. 1:11 ).
Yeyote aliyetamani kujichukulia juu yake jina la Kristo alijiunga na Kanisa la Mungu, Mos. 25:23 .
Wale wote waliokuwa waumini wa kweli katika Kristo walijichukulia juu yao jina la Kristo, Alma 46:15 .
Mlango wa mbinguni u wazi kwa wale watakaao katika jina la Yesu Kristo, Hel. 3:28 .
Heri yule apatikanaye kuwa yu mwaminifu katika jina langu ile siku ya mwisho, Eth. 4:19 .
Wako tayari kujichukulia juu yao jina la mwana, Moro. 4:3 (M&M 20:77 ).
Kuonekana kwa Kristo baada ya kifo
Yesu alipofufuka, kwanza alimtokea Maria, Mk. 16:9 (Yn. 20:11–18 ).
Yesu alitembea na kuzungumza na wawili kati ya wanafunzi wake katika barabara iendayo Emau, Lk. 24:13–34 .
Yesu aliwatokea Mitume, ambao walishikashika mikono na miguu yake, Lk. 24:36–43 (Yn. 20:19–20 ).
Yesu alimtokea Tomaso, Yn. 20:24–29 .
Yesu aliwatokea wanafunzi wake katika bahari ya Tiberia, Yn. 21:1–14 .
Yesu alihudumu kwa siku arobaini baada ya ufufuko wake, Mdo. 1:2–3 .
Stefano alimwona Yesu amesisima upande wa mkono wa kuume wa Mungu, Mdo. 7:55–56 .
Yesu alimtokea Sauli, Mdo. 9:1–8 (TJS, Mdo. 9:7 ; Mdo. 26:9–17 ).
Kristo alionekana kwa watu zaidi ya 500, 1 Kor. 15:3–8 .
Joseph Smith na Sidney Rigdon walimwona Yesu akiwa mkono wa kuume wa Mungu, M&M 76:22–23 .
Joseph Smith na Oliver Cowdery walimwona Bwana katika Hekalu la Kirtland, M&M 110:1–4 .
Kuwepo kwa Kristo kabla ya kuzaliwa duniani
Hapo mwanzo, Neno alikuwa pamoja na Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, na akakaa miongoni mwenu, Yn. 1:1, 14 (1 Yoh. 1:1–3 ).
Kabla Ibrahimu hajakuweko, MIMI niko, Yn. 8:58 .
Nitukuze mimi kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako, Yn. 17:5 .
Isaya amini alimwona Mkombozi wangu kama vile mimi na ndugu yangu Yakobo tulivyomwona, 2 Ne. 11:2–3 .
Kesho naja ulimwenguni, 3 Ne. 1:12–14 .
Kristo alikuwako kabla ya ulimwengu kuanza, 3 Ne. 26:5 (Yn. 6:62 ).
Kama nionekanavyo kwako ndivyo nitakavyoonekana kwa watu wangu katika mwili, Eth. 3:14–17 .
Mwana wangu Mpendwa, aliyekuwa Mpendwa wangu na Mteule tangu mwanzo, Musa 4:2 .
Bwana akasema: Nimtume nani? Na mmoja akasema kama Mwana wa Mtu: Niko hapa, nitume mimi, Ibr. 3:27 .
Yesu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, Mt. 7:28–29 (Mk. 1:22 ).
Mwana wa Mtu anao uwezo wa kusamehe dhambi hapa duniani, Mt. 9:6 .
Yesu aliamuru mapepo wachafu kwa mamlaka nao walimtii, Mk. 1:27 (Lk. 4:33–36 ).
Yesu aliwatawaza wale kumi na wawili wawe na uwezo, Mk. 3:14–15 .
Neno la Yesu lilikuwa na nguvu, Lk. 4:32 .
Baba amekabidhi hukumu zote kwa Mwana, Yn. 5:22, 27 .
Mungu alimpaka mafuta Yesu kwa Roho Mtakatifu na kwa uwezo, Mdo. 10:38 .
Kristo aliteuliwa kabla ya kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu, 1 Pet. 1:20 (Eth. 3:14 ).
Kristo anazo funguo za jehanamu na za mauti, Ufu. 1:18 .
Wanadamu wote wako chini ya Kristo, 2 Ne. 9:5 .
Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ndiye Baba wa mbingu na dunia, Mwumbaji wa vitu vyote tangu mwanzo, Hel. 14:12 .
Nimewapa ninyi mfano, Yn. 13:15 .
Mimi ndimi njia, kweli, na uzima, Yn. 14:6 .
Kristo pia aliteswa kwa ajili yetu, akituachia mfano, ili mfuate nyayo zake, 1 Pet. 2:21 .
Isipokuwa mtu amefuata mfano wa Mwana wa Mungu, aliye hai, hawezi kuokolewa, 2 Ne. 31:16 .
Ningelipenda muwe wakamilifu hata kama Mimi, 3 Ne. 12:48 .
Hivi daima zingateni kufanya, hata kama Mimi nilivyofanya, 3 Ne. 18:6 .
Nimeweka mfano kwa ajili yenu, 3 Ne. 18:16 .
Kazi ambazo mmeniona nikizifanya nanyi pia mtazifanya, 3 Ne. 27:21, 27 .
Wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo watakuwa kama yeye, Moro. 7:48 .
Mifano au ishara za Kristo
Habili alitoa sadaka ya wazao wa kwanza wa wanyama wake, Mwa. 4:4 (Musa 5:20 ).
Mchukue mwanao wa pekee Isaka, na ukamtoe sadaka, Mwa. 22:1–13 (Yak. [KM] 4:5 ).
Bwana aliwaamuru wana wa Israeli kutoa dhabihu wanakondoo wasio na ila, Ku. 12:5, 21, 46 (Hes. 9:12 ; Yn. 1:29 ; 19:33 ; 1 Pet. 1:19 ; Ufu. 5:6 ).
Huu ndiyo mkate ambao Bwana amewapa ninyi kula, Ku. 16:2–15 (Yn. 6:51 ).
Lipige jabali, nalo litatoa maji, ili watu wapate kunywa, Ku. 17:6 (Yn. 4:6–14 ; 1 Kor. 10:1–4 ).
Huyo mbuzi atajichukulia juu yake maovu yao yote, Law. 16:20–22 (Isa. 53:11 ; Mos. 14:11 ; 15:6–9 ).
Musa akamweka juu nyoka wa shaba nyeupe ili kuwaokoa wale watakaoitazama, Hes. 21:8–9 (Yn. 3:14–15 ; Alma 33:19 ; Hel. 8:14–15 ).
Yona alikuwa ndani ya tumbo la yule nyangumi kwa siku tatu, Yon. 1:17 (Mt. 12:40 ).
Unabii juu ya Kuzaliwa na Kifo cha Yesu Kristo
Samweli Mlamani alitoa unabii kuwa mchana, usiku, mchana wa mwanga; nyota mpya; na ishara nyinginezo, Hel. 14:2–6 .
Samweli Mlamani alitoa unabii kuhusu giza, mingurumo na radi, na kutetemeka kwa dunia, Hel. 14:20–27 .
Ishara za kuzaliwa kwa Yesu zilitimia, 3 Ne. 1:15–21 .
Ishara za kifo cha Yesu zilitimia, 3 Ne. 8:5–23 .
Ushuhuda uliotolewa juu ya Yesu Kristo
Paulo alishuhudia kwamba Yesu ndiye Kristo, Mdo. 18:5 .
Hata mapepo wabaya walishuhudia kwamba walimjua Yesu, Mdo. 19:15 .
Hapana mtu awezaye kusema kwamba Yesu ni Bwana isipokuwa kwa Roho Mtakatifu, 1 Kor. 12:3 .
Kila goti litapiga na kila ulimi utakiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, Flp. 2:10–11 .
Tulimwona na kusikia sauti ikimshuhudia kwamba yeye ndiye Mwana Pekee, M&M 76:20–24 .
Na huu ndiyo uzawa wa milele—kumjua Mungu na Yesu Kristo, M&M 132:24 .
Tunaamini katika Mungu Baba wa Milele, na katika Mwanawe, Yesu Kristo, M ya I 1:1 .
Tunaamini kwamba Kristo atatawala yeye mwenyewe duniani, M ya I 1:10 .
Utawala wa Kristo katika milenia
Mungu atampa Yesu kiti cha enzi cha Daudi baba yake, Lk. 1:30–33 .
Kristo atatawala milele na milele, Ufu. 11:15 .
Watakatifu watatawala pamoja na Kristo kwa miaka elfu moja, Ufu. 20:4 (M&M 76:63 ).
Mwana wa Mtu atakuja katika utukufu wa Baba yake, Mt. 16:27 .
Unitukuze mimi kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako, Yn. 17:5 .
Mtakatifu wa Israeli lazima atawale kwa utukufu mkuu, 1 Ne. 22:24 .
Tulikuwa na tumaini la utukufu wake, Yak. (KM) 4:4 .
Mwana wa Mungu yu aja katika utukufu wake, Alma 5:50 .
Alielezea mambo yote, kutoka mwanzo hadi atakapokuja katika utukufu wake, 3 Ne. 26:3 .
Mitume wangu watasimama wakiwa wamevikwa katika utukufu hata kama vile Mimi nilivyo, M&M 29:12 (M&M 45:44 ).
Tuliuona utukufu wa Mwana, katika mkono wa kuume wa Baba, M&M 76:19–23 .
Yohana aliona na kutoa shuhuda juu ya utimilifu wa utukufu wangu, M&M 93:6 (Yn. 1:14 ).
Uso wake ulingʼara kupita mwangaza wa jua, M&M 110:3 .
Utukufu wake ulikuwa juu yangu, nami nikauona uso wake, Musa 1:1–11 .
Hii ndiyo kazi yangu na utukufu wangu, Musa 1:39 .