Muziki Ona pia Imba; Wimbo Tuni na mipigo inayoimbwa na kuchezwa tangu nyakati za mwanzoni za biblia ili kuelezea shangwe, kusifu, na kuabudu (2Â Sam. 6:5). Yaweza kuwa katika namna ya sala. Zaburi huenda zilikuwa zikiimbwa kwa tuni rahisi na kuambatanishwa na vyombo. Miriamu, dada wa Haruni na Musa, akatwaa tari na yeye pamoja na wanawake wenzake wakacheza, Ku. 15:20. Walawi waliokuwa waimbaji walikuwa na matoazi na vinanda na makuhani mia moja ishirini walipuliza matarumbeta yao, 2Â Nya. 5:12. Yesu na wale Kumi na Wawili waliimba wimbo wa dini baada ya Karamu ya Mwisho, Mt. 26:30. Mkifundishana na kuonyana ninyi kwa ninyi kwa zaburi na wimbo, na tenzi za rohoni, Kol. 3:16. Je, mmejisikia kuimba wimbo wa upendo wa ukombozi, Alma 5:26. Nafsi ya Mungu hufurahia katika wimbo wa moyo, ndiyo, wimbo wa mwenye haki ni sala, M&M 25:12. Msifuni Bwana kwa kuimba, kwa muziki, na kwa kucheza, M&M 136:28.