Misaada ya Kujifunza
Mafarisayo


Mafarisayo

Katika Agano Jipya, ni kundi la kidini miongoni mwa Wayahudi ambao jina lao lilieleza kujitenga au tofauti. Mafarisayo walijisifia wao wenyewe juu ya kushika kikamilifu torati ya Musa na kujiepusha na kitu chochote kinachohusiana na Wayunani. Waliamini katika maisha baada ya kifo, Ufufuko, na kuwepo kwa malaika na roho. Waliamini kwamba sheria za mdomo na mila zilikuwa na umuhimu sawa kama sheria zilizoandikwa. Mafundisho yao yaliipunguza dini kuwa kitu cha kutii kanuni na walihimiza kiburi cha kiroho. Walisababisha watu wengi wa Kiyahudi kumtilia mashaka Kristo na injili yake. Bwana aliwakana Mafarisayo na matendo yao katika Mathayo 23; Marko 7:1–23; na Luka 11:37–44.