Kuhani mkuu, nabii, na kiongozi katika Agano la Kale aliyeishi baada ya Gharika na katika wakati wa Ibrahimu. Aliitwa mfalme wa Salemu (Yerusalemu), mfalme wa amani, mfalme wa haki (ambayo kwa Kiebrania ndiyo maana ya neno Melkizedeki), na kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana.