Utovu wa maadili ya kujamiiana Ona pia Kupenda anasa, Matamanio ya anasa; Uasherati; Uzinzi Kushiriki katika uzinzi kwa makusudi, uasherati, tabia za ubasha na usagaji, kujamiiana kwa maharimu, au nyingine yoyote isiyo takatifu, isiyo ya kawaida, au mambo ya kujamiiana yasiyo safi. Haya na tumnyweshe baba yetu mvinyo, na tukalale naye, Mwa. 19:30–36. Reubeni akaenda na akalala na Bilha suria wa baba yake, Mwa. 35:22 (Mwa. 49:4; 1 Nya. 5:1). Tabia za ubasha na utovu mwingine wa kujamiiana ni chukizo, Law. 18:22–23. Kama mwanamume atalazimisha mwanamke kulala naye, ni yule mwanamume tu ndiye aliye na hatia ya dhambi, Kum. 22:25–27. Yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake, Mt. 5:28 (3 Ne. 12:28). Uasherati, uchafu, tamaa mbaya ndiyo ibada ya masanamu, Kol. 3:5. Katika siku za mwisho wanadamu watakuwa hawana upendo wa asili, 2 Tim. 3:1–3. Dhambi ya kujamiiana ni chukizo, Alma 39:3–5.