Tabia ya Ubasha Ona pia Kupenda anasa, Matamanio ya anasa; Uzinzi Mahusiano ya kujamiana kwa watu wa jinsia moja. Mungu anakataza shughuli za kujamiana za aina hii. Walete nje kwetu sisi, ili tupate kuwajua, Mwa. 19:1–11 (Musa 5:51–53). Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo, Law. 18:22 (Law. 20:13). Pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli, Kum. 23:17. Watangaza dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi, Isa. 3:9 (2 Ne. 13:9). Wanaume waliwakiana tamaa wao kwa wao, Rum. 1:27. Wajitukanao wenyewe kwa kujamiana hawataurithi ufalme wa Mungu, 1 Kor. 6:9–10. Sheria haikutungwa kwa ajili ya mtu mwenye haki, bali kwa ajili ya wale wajichafuao wenyewe kwa kujamiana wanaume wa jinsia moja, 1 Tim. 1:9–10. Watu waendao kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili wamewekwa kuwa mfano, watateseka kisasi cha moto wa milele, Yuda 1:7.