Baraza Mbinguni Ona pia Maisha kabla ya kuzaliwa; Mpango wa Ukombozi; Vita Mbinguni Tukio katika maisha yetu kabla ya kuzaliwa hapa duniani wakati Baba alipotoa mpango Wake kwa watoto Wake wa kiroho ambao wangekuja katika dunia hii. Na wana wa Mungu walipopiga kelele kwa shangwe, Ayu. 38:4–7. Nitakiinua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu, Isa. 14:12–13. Palikuwa na vita mbinguni, Ufu. 12:7–11. Kabla hawajazaliwa, walipata masomo yao ya awali katika ulimwengu wa Roho, M&M 138:56. Shetani aliasi katika maisha ya kabla ya kuzaliwa hapa duniani, Musa 4:1–4. Viumbe-akili-asilia viliumbwa kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, Ibr. 3:22. Na Miungu wakashauriana wenyewe, Ibr. 4:26. Miungu wakamaliza kazi waliyoshauriana kuifanya, Ibr. 5:2.