Ufahamu Ona pia Hekima; Maarifa; Ukweli Kupata maarifa juu ya au kutambua maana ya ukweli fulani, ikijumuisha matumizi yake katika maisha. Usitegemee ufahamu wako mwenyewe, Mit. 3:5. Katika kupata kwako kote jipatie ufahamu, Mit. 4:7. Yesu alisema kwa mifano na baadhi hawakufahamu, Mt. 13:12–17. Bwana alifungua ufahamu wao, Lk. 24:45. Kama hamwezi kufahamu maneno haya, itakuwa ni kwa sababu hamuombi, 2 Ne. 32:4 (3 Ne. 17:3). Kumbukumbu ilitunzwa ili kwamba tupate kuisoma na kufahamu, Mos. 1:2–5. Kwa sababu ya kutokuamini kwao, hawakuweza kufahamu neno la Mungu, Mos. 26:3. Walikuwa watu wenye ufahamu mkamilifu, Alma 17:2–3. Neno lile lilianza kuangaza ufahamu wangu, Alma 32:28. Njooni tusemezane ili mpate kufahamu, M&M 50:10–12, 19–23. Wazazi lazima wawafundishe watoto wao kufahamu, M&M 68:25. Matendo na miujiza ya Mungu yaweza tu kufahamika kwa njia ya Roho Mtakatifu, M&M 76:114–116. Shetani hutafuta kuigeuza mioyo ya wanadamu mbali na ufahamu, M&M 78:10. Nuru ya Kristo huhuisha ufahamu wetu, M&M 88:11.