Giza, Kiroho Ona pia Ovu, Uovu Uovu au ujinga wa mambo ya kiroho. Ole wao watiao giza badala ya nuru, Isa. 5:20 (2 Ne. 15:20). Giza litaifunika dunia, na giza kuu litawafunika watu, Isa. 60:2. Yesu atatoa nuru kwa wale wakaao gizani, Lk. 1:79. Nuru yangʼaa gizani, na giza halikuiweza, Yn. 1:5 (M&M 45:7). Tuyavue matendo ya giza na kuzivaa silaha za nuru, Rum. 13:12. Msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, Efe. 5:8–11. Kwa sababu ninyi hamuombi, hamjaletwa kwenye nuru lakini lazima mwangamie gizani, 2 Ne. 32:4. Shetani hueneza matendo ya giza, Hel. 6:28–31. Nguvu za giza zinaenea juu ya dunia, M&M 38:8, 11–12. Ulimwengu wote unagumia chini ya giza na dhambi, M&M 84:49–54. Kama jicho lako likiwa tu katika utukufu wangu, hapatakuwa na giza ndani yako, M&M 88:67. Matendo ya giza yalianza kuenea miongoni mwa wana wote wa watu, Musa 5:55.