Utaratibu Mfano ambao mtu anaweza akafuata ili kupata matokeo fulani. Katika maandiko, utaratibu kwa kawaida humaanisha mfano wowote kwa ajili ya kuishi njia fulani au kwa ajili ya kujenga kitu fulani. Bwana aliwaamuru Israeli kujenga hema takatifu kulingana na utaratibu ulioonyeshwa kwa Musa, Ku. 25. Daudi alimpa Suleimani utaratibu wa ujenzi wa hekalu, 1 Nya. 28:11–13. Katika mimi Yesu Kristo apate kuonyesha mfano kwa wale watakaomwamini, 1 Tim. 1:16. Nitatoa kwenu utaratibu katika mambo yote, ili msidanganyike, M&M 52:14.