Misaada ya Kujifunza
Damu


Damu

Huchukuliwa na Waisraeli wa zamani na tamaduni nyingi za leo kama chanzo muhimu cha uhai au nguvu muhimu kwa uzima wa wenye mwili wote. Katika nyakati za Agano la Kale Bwana aliwakataza Israeli wasile damu kama chakula (Law. 3:17; 7:26–27; 17:10–14).

Uwezo wa kulipia dhambi kwa dhabihu ulikuwa katika damu kwa sababu damu ilichukuliwa kama kitu muhimu katika uzima. Dhabihu za wanyama wakati wa Agano la Kale ilikuwa ishara ya dhabihu kuu ambayo baadaye ilifanywa na Yesu Kristo (Law. 17:11; Musa 5:5–7). Damu ya kulipia dhambi ya Yesu Kristo humsafisha mwenye kutubu kutokana na dhambi (1 Yoh. 1:7).