Yohana Mbatizaji Ona pia Elia; Ukuhani wa Haruni Mwana wa Zakaria na Elizabethi katika Agano Jipya. Yohana alitumwa kuwaandaa watu kwa kumpokea Masiya (Yn. 1:19–27). Alishikilia funguo za Ukuhani wa Haruni na alimbatiza Yesu Kristo. Isaya na wengineo walitoa unabii juu ya huduma ya Yohana, Isa. 40:3 (Mal. 3:1; 1 Ne. 10:7–10; 2 Ne. 31:4). Aliwekwa gerezani na akakatwa kichwa, Mt. 14:3–12 (Mk. 6:17–29). Gabrieli alitangaza kuzaliwa na huduma ya Yohana kwa Zakaria, Lk. 1:5–25. Yesu alifundisha kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa nabii mkuu, Lk. 7:24–28. Alimtambua Yesu kama ni Mwana wa Mungu, Yn. 1:29–34. Wanafunzi wa Yohana wakaja kuwa wanafunzi wa Yesu, Yn. 1:25–29, 35–42 (Mdo. 1:21–22). Hakufanya muujiza, Yn. 10:41. Kama mtu mfufuka, alitumwa kuwatawaza Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Ukuhani wa Haruni, M&M 13 (M&M 27:7–8; JS—H 1:68–72). Alitawazwa na malaika wakati alipokuwa na umri wa siku nane, M&M 84:28.