Hubiri Ona pia Injili; Kazi ya kimisionari Kutoa ujumbe ambao hutoa ufahamu bora juu ya kanuni au mafundisho ya injili. Bwana amenipaka mafuta niwahubirie habari njema wanyenyekevu, Isa. 61:1 (Lk. 4:16–21). Inuka, uende Ninawi, na ukawahubirie, Yona 3:2–10. Tangu saa ile Yesu alianza kuhubiri, Mt. 4:17. Enendeni ulimwenguni kote, na mkaihubiri injili kwa kila kiumbe, Mk. 16:15. Sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa, 1 Kor. 1:22–24. Alikwenda na akazihubiria Roho zilizokuwa kifungoni, 1 Pet. 3:19. Hapakuwa na chochote isipokuwa kulikuwa na kuhubiri na kuwachochea ili daima wawe katika woga wa kumwogopa Mungu, Eno. 1:23. Aliwaamuru wasihubiri chochote isipokuwa toba na imani juu ya Bwana, Mos. 18:20. Kuhubiriwa kwa neno kulikuwa na uelekeo mkubwa wa kuwaongoza watu kufanya yale yaliyo ya haki, Alma 31:5. Hupaswi kudhani ya kuwa umeitwa kuhubiri hadi pale unapoitwa, M&M 11:15. Haitatolewa kwa yeyote kwenda kuhubiri injili isipokuwa ametawazwa, M&M 42:11. Injili hii itahubiriwa kwa kila taifa, M&M 133:37. Injili ilianza kuhubiriwa tangu mwanzo, Musa 5:58.