Maarifa Ona pia Hekima; Ufahamu; Ukweli Ufahamu na uelewa, hususani wa ukweli kama ulivyofundishwa au kuthibitishwa na Roho. Bwana ni Mungu wa maarifa, 1 Sam. 2:3. Bwana ni mkamilifu, katika maarifa, Ayu. 37:16. Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Mit. 1:7. Yule mwenye maarifa huyazuia maneno yake, Mit. 17:27. Dunia itajawa na kumjua Bwana, Isa. 11:9 (2 Ne. 21:9; 30:15). Mmeuondoa ufunguo wa maarifa, Lk. 11:52. Upendo wa Kristo wapita ufahamu, Efe. 3:19. Katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, 2 Pet. 1:5. Nefi alikuwa na ufahamu mkubwa wa wema wa Mungu, 1 Ne. 1:1. Watakapomfahamu Mkombozi wao, 2 Ne. 6:11. Wenye haki watakuwa na ufahamu ulio kamili wa uadilifu wao, 2 Ne. 9:14. Roho hutupa maarifa, Alma 18:35. Ufahamu wenu ni mkamilifu katika lile jambo, Alma 32:34. Walamani watarejeshwa katika ufahamu wa kweli wa Mkombozi wao, Hel. 15:13. Mpate kujua kwa ufahamu ulio kamili kuwa ni ya Mungu, Moro. 7:15–17. Watakatifu watapata hazina kubwa ya maarifa, M&M 89:19. Maarifa safi huikuza sana nafsi, M&M 121:42. Mtu aliye na funguo za ukuhani mtakatifu hana ugumu katika kupata maarifa ya kweli, M&M 128:11. Kama mtu anapata maarifa katika maisha haya, atakuwa na heri katika ulimwengu ujao, M&M 130:19. Haiwezekani kuokolewa katika ujinga, M&M 131:6.