Misaada ya Kujifunza
Lehi, Baba wa Nefi


Lehi, Baba wa Nefi

Katika Kitabu cha Mormoni, ni nabii Mwebrania aliyeiongoza familia yake na waliomfuata kutoka Yerusalemu hadi nchi ya ahadi katika Marekani yapata mwaka 600 K.K. Lehi alikuwa ndiye nabii wa kwanza miongoni mwa watu wake katika Kitabu cha Mormoni.

Lehi alitoroka Yerusalemu pamoja na familia yake kwa amri ya Bwana (1 Ne. 2:1–4). Alikuwa ni wa uzao wa Yusufu, aliyeuzwa Misri (1 Ne. 5:14). Bwana alimpa ono la mti wa uzima (1 Ne. 8:2–35). Lehi na wanawe walijenga mashua na wakasafiri hadi Marekani (1 Ne. 17–18). Yeye na wazao wake wakastawi katika nchi mpya (1 Ne. 18:23–25). Kabla ya kufa, Lehi aliwabariki wanawe na aliwafundisha juu ya Kristo na juu ya kutokea kwa Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho (2 Ne. 1:1–4:12).

Kitabu cha Lehi

Joseph Smith alianza na Kitabu cha Lehi wakati alipokuwa akitafsiri Kitabu cha Mormoni. Ilikuwa ni historia ambayo Mormoni aliifanyia ufupisho kutoka katika mabamba ya Lehi. Baada ya kupata kurasa 116 za muswada uliotafsiriwa kutoka katika kitabu hiki, Joseph alimpa muswada Martin Harris, ambaye kwa muda mfupi alitumika kama mwandishi wa Joseph katika tafsiri ya Kitabu cha Mormoni. Kurasa hizi ndizo zilipotezwa. Joseph hakurudia kutafsiri tena kitabu cha Lehi ili kufidia zile zilizopotea lakini badala yake alitafsiri historia nyingine inayofanana nayo kutoka katika mabamba ya dhahabu (ona utangulizi wa M&M 3; 10). Historia hizi nyingine ndivyo vitabu sita vya mwanzo vya Kitabu cha Mormoni.